Habari za michezo

MWISHO WA TETESI….HABIB KYOMBO ATUA SINGIDA BIG STAR….MASHABIKI SIMBA WASHUSHA PUMZI….

admin June 21, 2022 11:59 am


Mshambuliaji Habib Kyombo amekua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Singida Big Stars itakayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2022/23.

Kyombo anayemalizia mkataba wake Mbeya Kwanza FC, amekamilisha dili la kujiunga na klabu hiyo, leo Jumanne (Juni 21) mchana, kisha kuthibitishwa kupitia katika Kurasa za Mitandao ya Kijamii za Singida Big Stars.

Mchezaji huyo ambaye alibahatika kusajiliwa Mamelodi Sondowns ya Afrika Kusini, alihusishwa kujiunga na Simba SC mwishoni mwa juma lililopita, hivyo kusajiliwa Singida Bid Stars kunasitisha tetesi hizo ambapo mashabiki wengi wa Simba kwenye mitandao walikuwa wakiponda kuwa staa huyo wa zamani wa Mbao hana hadhi ya kusajiliwa na kikosi chao.

Mara baada ya taarifa ya usajili wa nyota huyo kutoka rasmi leo,mashabiki wengi wa timu hiyo walionekana kuridhika na kufurahi kuwa straika huyo hajiungi na Simba kama ilivyotarajiwa.

Taarifa za Singida Big Stars za kuthibitisha kumsajili Mshambuliaji huyo zilizotolewa kwenye ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo zimeeleza:

RASMI: Habib Kyombo ni BIG STAR ⭐️

Karibu fundi wa mpira uitumikie klabu yako pendwa katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2022/2023).


KISA USAJILI WA MORRISON ….SALEH JEMBE AZICHANA SIMBA NA YANGA…ATAKA MIL 20 IMALIZE UTATA WOTE… MNIGERIA WA COASTAL UNION AIPOTEZEA SIMBA…ADAI NI JAMBO LA ‘KIPUUZI’ KUIJADILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply