Habari za michezo

WAWA NAYE APITISHIWA FAGIO LA CHUMA SIMBA…KUAGWA KIULAYA ULAYA YANI…MTIBWA SUGARA WATAJWA….

admin June 21, 2022 8:38 am


BAADA ya kuitumikia klabu ya Simba kwa misimu minne, Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao ambapo mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu huku mchezo wa Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho.

Simba imethibitishi kuachana na beki huyo raia wa Ivory Coast aliyejiunga na Simba mwaka 2018 akitokea Azam FC leo Juni 21, 2022.

Pascal Wawa hakuwa na msimu mzuri ukilinganisha na misimu iliyopita huku ujio wa beki Mkongo Enock Inonga ukifanya nafasi yake kuwa finyu ndani ya kikosi cha Simba  mara nyingi akisotea benchi.

Katika kipindi alichokaa kikosini hapo Wawa amekuwa akicheza eneo la safu ya ulinzi akiisaidia na Joash Onyango, Kennedy Juma pamoja na Henoc Inonga.

Wawa ni mchezaji wa tatu kuagwa na Simba baada ya Bernard Morrison pamoja na Rally Bwalya aliyeangwa hivi karibuni.

BWANA WEEE…KUMBE ULE MPANGO WA AZAM FC KWA LAMINE MORO UKO NAMNA HII….MAMBO NI KIMYA KIMYA MZEE BABA… MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA JULIO NA NAMUNGO YAKE…AUKATAA UBINGWA YA YANGA….ADAI BINGWA NI SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply