Habari za michezo

BAADA YA BWALYA KUAGWA SIMBA JUZI..KAONA ISIWE TABU AISEE…KAANIKA HAYA MENGINE YA MOYONI..

admin June 22, 2022 2:35 am


KIUNGO wa kimataifa wa Zambia, Rally Bwalya, juzi Jumapili alicheza mchezo wa mwisho dhidi ya KMC wa Ligi Kuu Bara akiwa Simba baada ya kuitumikia kwa kipindi cha misimu miwili.

Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 akitokea Power Dynamos ya Zambia akisaini mkataba wa miaka mitatu. Katika mchezo wa juzi uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Simba ilishinda 3-1.

Kiungo huyo anaondoka Simba akiwa amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja baada ya Amazulu ya Afrika Kusini kufanikiwa kumsajili.

Baada ya mchezo huo, Bwalya alisema: “Mchezo wa mwisho. Nalazimika kusema kwa heri kwa watu wangu wote ninaowapenda.

“Siku yangu ya mwisho kama mchezaji wa Simba SC imekuwa ya hisia kubwa sana, asante kwa kuniaga kwa ushindi. Ninathamini mapenzi, bila shaka nitawamisi kila siku. Asanteni sana.”

USAJILI WA MNIGERIA SIMBA NI KAMA MUVI LA KIJASUSI AISEE…AZAM WAZIDIWA KIDOGO SANA KUMNYAKUA JUU KWA JUU… WATAKAOENDA KUTAZAMA KOMBE LA DUNIA QATAR WAZUIWA KUFANYA NGONO NA KUNYWA POMBE…ADHABU NI JELA AU KIFO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply