Semaji la Yanga SC, Haji Manara amesema kiungo wao mshambuliaji Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kama timu ikimuhitaji, inatakiwa iweke mezani pesa zisizopungua shilingi bilioni 1.
Manara amefunguka hayo leo Juni 22, 2022 alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha habari cha jijini Dar.
โMchezaji kama Feisal sasa hivi ana mkataba, inakuja Klabu labda kutoka South Afrika inakuletea ofa ya USD 50,000 au USD 100,000 hatuwezi kukataa kuzungumza naye huyu mtu.
โHapa katikati zimekuja ofa za baadhi ya timu, hatuwezi kumuuza Feisal Chini ya Tsh. Bilioni 1 sawa na kama USD 500,000 hapo angalau tunaweza kuzungumza,โ alisema Manara.