Habari za michezo

HUYU HAPA MTANZAMIA ALIYENGIA KWENYE REKODI ZA AL AHLY YA MISRI…ALICHOFANYA CHAWEKA HISTORIA…

admin June 24, 2022 7:39 am


Nyota wa kimataifa wa Tanzania Himid Mao ‘Ninja’ anayechezea klabu ya Ghazl Mahalla ya nchini Misri ameendeleza moto wake baada ya kuifungia timu yake bao la kufutia macho dhidi ya Al Ahly walipoambulia kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo.

Himid aliifungia timu yake bao la kusawazisha mnamo dakika ya 57 ambapo walikuwa nyuma kwa bao moja kisha bao likaresha matumaini ya klabu yake kuondoka na ushindi hadi hapo  Al Ahly walipoumaliza mchezo kwa kufunga bao la pili dakika za mejeruhi na mchezo ukamalizika kwa Al Ahly kuondoka na pointi tatu.

Nyota huyo wa Tanzania amekua akiiongoza safu ya kiungo ya Ghazl Mahalla ambapo hadi hivi tayari amecheza mechi 20 katika 21 msimu huu akiwa na timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa Himidi Mao alishawahi kuichezea Azam Fc klaba ya kutimkia nchini Misri na kwenda kuungana na Petrojet, Enppi Sc pamoja Entag El Harby zote zikiwa za nchini Misri. 

KISA BWALYA KUSEPA BONGO…STRAIKA KMC AIBUKA NA HILI…ATUMA MAOMBI MAZITO KWA SIMBA SC KIUNGO MKENYA ATUA BONGO KIMYA KIMYA…AIFUATA SIMBA AKIWA NA BARUA YA WASAUZI…DILI LIKIFELI ANASEPA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply