Habari za michezo

KIUNGO MKENYA ATUA BONGO KIMYA KIMYA…AIFUATA SIMBA AKIWA NA BARUA YA WASAUZI…DILI LIKIFELI ANASEPA….

admin June 24, 2022 12:17 pm


Winga wa kimataifa Mkenya Harrison Mwendwa amewasili nchini asubuhi ya leo akitokea mapumzikoni nchini kwao baada ya Ligi ya Zambia kumalizika akicheza katika klabu ya Kabwe Warrios.

Inaelezwa Mwendwa amewasili hapa nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kimkataba na Simba iliyoonyesha nia ya kumuhitaji tangu dirisha dogo la msimu huu mwezi Januari.

Taarifa inaeleza kama Mwendwa atakubaliana na Simba katika mazungumzo hayo atasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo na kama mambo hayatakwenda vizuri atafanya maamuzi mengine kwani kuna timu zinamuhitaji hapa nchini na Afrika Kusini.

Winga huyo anayetumia mguu wa kushoto aliwahi kutamba na timu za Mathare United, Kariobangi Sharks na AFC Leopards amekuwa akiwindwa na Simba tangu kwenye dirisha dogo la usajil la msimu huu .

HUYU HAPA MTANZAMIA ALIYENGIA KWENYE REKODI ZA AL AHLY YA MISRI…ALICHOFANYA CHAWEKA HISTORIA… ULE MSELELEKO WA DStv WIKIEND HII UNAKUJIA NA MAJAMAA WA WATUBAKI…USIPOCHEKA UNASHIDA YA BANDAMA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply