BIashara United

WAKATI SIMBA WAMESHAWAAGA WAWA NA BWALYA…REDONDO NAYE AWAAGA BIASHARA UTD MAPEMA…UELEKEO WAKE HUU..

admin June 24, 2022 3:37 am


Kiungo Mshambuliaji Ramadhan Chombo ‘Redondo’ ameweka wazi ataachana na Biashara United Mara mwishoni mwa msimu huu, baada ya kumaliza mkataba wake.

Redondo ametoa kauli hiyo, huku Biashara United Mara ikibakisha michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, ikiwa katika hali mbaya ya kuchungulia shimo la kushuka daraja.

Amesema tayari ameshapata klabu ya kuitumikia msimu ujao, lakini anasubiri siku na saa maalum, ili kuweka wazi kwa ajili ya mashabiki wake ambao wana hamu ya kujua wapi atakapocheza msimu ujao.

“Msimu ujao nitakuwa timu nyingine, tuombe uzima tu. siwezi kutaja timu kwa sasa kwani bado nipo Biashara United Mara na ligi hajiamalizika, ila siku si nyingi nitasema,” amesema Redondo.

Ramadhan Chombo ‘Redondo’ alisajiliwa Biashara United Mara misimu mitatu iliyopita, na kwa kipindi chote ameonyesha kuwa na kiwango bora, ambacho kilikua msaada mkubwa kwa timu hiyo ya mjini Musoma-Mara.

KISA SIMBA KUMZUIA MORRISON…YANGA WASHINDWA KUJIZUIA…BUMBULI AIBUKA NA KUJIBU MAPIGO…”IWE ISIWE TUTAMSAJILI”… BAADA YA KUUWASHA MOTO VILIVYO ….MATOLA AIBUKA NA HILI KUHUSU BANDA NA SAKHO…AFUNGUKA CHANZO CHA KUFELI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply