KLABU ya Yanga imetoa rasmi ratiba yao ya kusherehekea ubingwa kwa kuanza kulipokea Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Yanga jana saa 10:00 jioni ilicheza mchezo wake wa 29 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine, Mbeya na ndipo itakapokabidhiwa rasmi Kombe hilo na baada ya hapo kesho wataanza rasmi kurejea Dar.
Kwa mujibu wa ratiba Yanga itawasili katika uwanja wa Mwl Nyerere saa 5 Asubuhi na msafara utaanza kuondoka uwanja wa ndege saa 5:30 Asubuhi.
Saa 6 mchana viongozi wa Matawi na Wazee wa Jangwani kuwasili makao makuu na saa 8 mchana timu itawasili makao makuu Jangwani.
Saa 8:15 Dua Wazee na Wachezaji na 8:30 Wachezaji watapanda juu ya jengo la makao makuu kuonyesha kombe kisha saa 9 Alasiri chakula cha mchana.
Saa 9:30 Alasiri timu itaondoka Jangwani kwenda Samora na saa 10 Alasiri timu itawasili Salamander Towe kisha kutakuwa na Burudani mpaka saa 11:00 jioni kutoka kwa wasanii, Juma Nature, Madee, Marioo na Mzee wa Bwax.
Saa 12:30 jioni timu itafungua shampeni na saa 1:00 usiku watafyatua mafataki kwa kuashiria ni mwisho wa sherehe.