Habari za michezo

WAKICHEZA DHIDI YA TANZANIA PRISONS LEO..BOCCO NA MKUDE WALIAMSHA SIMBA…MATOLA ATOA TAMKO HILI…

admin June 26, 2022 7:00 am


Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Seleman Matola amesema Nahodha John Bocco na kiungo Jonas Mkude ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri kuelekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa leo wa ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons.

Matola ameyasema hayo akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) muda mfupi kabla ya kupaa kuelekea Mbeya huku akisema wachezaji wengine wote pia wapo kwenye hali nzuri.

Nahodha Bocco yeye alishaanza kuonekana akiwa benchi katika mechi mbili zilizopita lakini Mkude amekosekana muda mrefu kutokana na kuwa na majeruhi lakini sasa yupo kamili kuipigania timu.

Matola amesema tumeamua kuondoka siku moja kabla ya mchezo kwa kuwa tunajua Uwanja wa Sokoine una mechi nyingine kwa hiyo hata kama tungewahi tusingepata nafasi ya kufanya mazoezi hivyo tulifanya Mo Arena asubuhi ndio tukaanza safari.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, mara zote tukikutana na Prisons mechi inakuwa ngumu hasa wakiwa Sokoine lakini safari hii itakuwa ngumu zaidi sababu hawapo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo hivyo watataka kupata pointi tatu kutoka kwetu lakini tupo tayari kuwakabili,” amesema Matola.

Matola amesema katika mchezo wa leo tutawakosa mlinda mlango Aishi Manula (ana matatizo ya kifamilia), Pape Sakho (ameumia bega) na Sadio Kanoute (ameenda nchini kwao kufuatilia passport yake ambayo imeisha muda wake).

MSUVA AJIPELEKA MWENYEWE YANGA….AFUNGUKA SIMBA WALIVYOMSUMBUA ZAIDI YA MARA 5…GSM WAFANYA KWELI… DILI LA MSUVA KUTUA YANGA SI MCHEZO AISEE…GSM WAMWEKEA MEZANI MIL 350…NABI APAGAWA KWA MAVITU YAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply