Habari za michezo

AHMED ALLY: SIMBA INGESHINDA UBINGWA LIGI KUU..TUSINGEPATA HATA MASHABIKI 20 WAKUTUPOKEA NA KOMBE…

admin June 27, 2022 5:32 pm


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ameipiga kijembe Young Africans, kufuatia mapokezi makubwa iliyoyapata jana Jumapili (Juni 26), jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Young Africans kilipokewa kishujaa na Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kikitokea jijini Mbeya, ambako kilikabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Tanzania Bara, baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City FC.

Ahmed amesema hana budi kuipongeza Young Africans kwa mafanikio ya kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara, lakini anaamini kufurika kwa Mashabiki katika mapokezi ya timu yao, kumetokana na ukame wa miaka mitano ambayo ilishuhudia wakimaliza mikono mitupu.  

Amesema anaamini ingekuwa upande wa Simba SC, mapokezi yasingekua ya mafuriko kama ilivyokua jana Jumapili (Juni 26), kwani Mashabiki na Wanachama wao wameshazoea Ubingwa.

“Nawapongeza Yanga SC kwa kufurika, najua wamefurika kwa sababu wana ukame wa miaka mitano. Tungebeba sisi hata watu 20 usingewaona uwanja wa ndege maana tushazoea” Ahmed Ally

Young Africans imetwaa ubingwa wake wa kwanza baada ya kutoka kapa kwa misimu minne mfululizo, huku ikiaacha Simba SC patupu msimu huu.

TOKA AFUKUZWE…KWA MARA YA KWANZA  KABWILI AIBUKA NA KUANIKA YOTE KUHUSU YANGA…”MMENIKOMAZA”…. GEITA GOLD WANOGEWA NA DUCHU…MIKAKATI YAFANYWA KIMYA KIMYA KUEPUSHA SHARI ZA SIMBA NA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply