Habari za michezo

KIUNGO MPYA SIMBA AMALIZA LIGI YA GHANA KWA MKOSI…SIKU YA KUTAMBULISHWA MSIMBAZI YATAJWA…

admin June 27, 2022 5:58 pm


Imefahamika kuwa Kiungo Mshambuliaji mpya wa Simba SC Augustine Okrah, atawasili jijini Dar es salaam baada ya kuitumikia klabu ya Bechem United katika mchezo wa mwisho wa msimu wa 2021/22.

Okrah jana Jumapili (Juni 26) aliitumikia Bechem United katika mchezo wa Fainali Kombe la FA nchini Ghana, na klabu yake ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Accra Hearts of Oak.

Hata Hivyo Okrah hakumaliza vizuri msimu wa 2021/22, kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo, baada ya kupinga maamuzi ya mshika kibendera.

Taarifa zinasema kuwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, atatambulishwa rasmi kwa Wanachama na Mashabiki wa Simba SC, baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya Kwanza, utakaopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Okrah amesaini mkataba wa miaka miwili na Uongozi wa Simba SC, baada ya kufanya mazungumzo binafsi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Agin’ aliyefunga safari hadi Ghana.

GEITA GOLD WANOGEWA NA DUCHU…MIKAKATI YAFANYWA KIMYA KIMYA KUEPUSHA SHARI ZA SIMBA NA YANGA… TUNZA TEREHE 30 YANGA WANAJAMBO LAO ZITO…VIFAA VIPYA KUANZA KUMIMINIKA KWA MFUMO WA LUKU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply