Habari za michezo

PAMOJA NA KUITIKISA NCHI JANA KWA GWARIDE LA UBINGWA….YANGA WAKAZANIA KUIFIKIA REKODI HII YA SIMBA…

admin June 27, 2022 12:39 pm


Kikosi cha klabu ya Yanga kinarejea leo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa mwisho wa kufungia msimu dhidi ya Mtibwa Sugar mnamo June 29, 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa kumi kamili jioni.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga Hassani Bumbuli amesema bado wana kiu ya kusaka rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa kimashindano huku kikosi hicho kikitarajiwa kuanza mazoezi rasmi mnamo siku ya Jumanne asubuhi ya June 28,2022.

“Ni mchezo muhimu sana wa kuandika historia,kuna timu ziliweka historia nyuma lakini sisi hatujapoteza katika mashindano yoyote na tunataka kuweka historia ya kumfunga Mtibwa Sugar ili twende tukamalize msimu vizuri  Arusha kwenye fainali ya FA”amesema Bumbuli

Mzunguko wa 30 wa ligi kuu Tanzania Bara 2021/22 unatarajiwa kuhitimishwa kwa michezo 8 kuchezwa kwa muda mmoja majira ya saa kumi kamili jioni mnamo June 29,2022 huku klabu ya Mbeya Kwanza kutokea jijini Mbeya ikiwa klabu ya kwanza kushuka daraja kwa msimu huu.

Simba na Azam pekee ndiyo zinarekodi ya kucheza msimu mzima wa mashindano ya Ligi Kuu bila kuruhusu kufungwa hata mechi mmoja, ambapo pia katika misimu hiyo miwili tofauti timu hizo zilitawa ubingwa.

KISA PURUKUSHANI ZA USAJILI BONGO….SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI RASMI KWA MASHABIKI WOTE NCHINI… RUNGU LA FIFA LAWAFANYA GEITA GOLD KUITANA KUMJADILI NDAYIRAGIJE..WADAI KUNA VIFUNGU VYA KIMKATABA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply