Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga Nasreddine Nabi amesema mapokezi waliyoyafanya mashabiki wa timu hiyo yamejenga historia kwenye maisha yake ya soka.
Yanga jana walitua wakitokea Mbeya walikokabidhiwa taji la ubingwa wa msimu huu na kupokelewa na umatiwa mashabiki uliomstua kocha Nabi.
“Kwenye maisha yangu ya soka tangu nimeanza kufundisha sijawahi kushuhudia umati mkubwa wa mashabiki kama ilivyotokea jana nimejengewa historia mpya,” anasema Nabi na kuongeza.
“Nawashukuru wana Yanga wote mashabiki, viongozi na wachezaji kwa ushirikiano mkubwa tuliouonyesha na kuzaa furaha ya wananchi wengi wenye mapenzi ya soka bado tunasafari ndefu nahitaji ushirikiano zaidi”. anasema.
Naye nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amewashukuru Wanayanga wote kwakuwapokea kwa nderemo na anatarajia mengi zaidi kutoka kwao kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).
“Mapokezi waliyoyafanya Wanayanga ni yamenipa picha nyingine kabisa nimeshudia mashabiki wengi lakini kwa umati wa jana kwenye maisha yangu sijawahi kushuhudia namuomba Mungu atujaalie mshikamano katika safari yetu.” anasema Nondo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha amesema historia imeandikwa hii ni kauli baada ya mapokezi makubwa waliyoonyeshwa na mashabiki wa timu hiyo.