Habari za Simba
Habari za michezo

MASTAA WALIOPIGWA PANGA SIMBA KUPETA NA TIMU HIZI ZA LIGI KUU…

admin January 15, 2024 8:32 pm

NYOTA watatu kati ya sita waliotemwa na Simba katika dirisha dogo, Nassor Kapama, Jimmyson Mwanuke na Shaaban Idd Chilunda wamepata dili baada ya kunaswa na Mtibwa Sugar na KMC.

Mwanuke na Kapama wametua zao Mtibwa, wakati Chilunda aliyewahi kuwika na Azam FC akisajiliwa KMC ili kuendeleza moto alioshindwa kuuwasha Msimbazi.

Kapama alisema ni kweli amemalizana na Mtibwa kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuvunjiwa mkataba na Simba sasa atakuwa huko kuipambania timu hiyo isishuke daraja.

“Nimemalizana na Mtibwa nitacheza huko kwa miezi sita naamini ni chaguo sahihi baada ya ofa nyingi nilizokuwa nazo naamini nitapambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuiondoa timu hiyo kwenye hatari ya kushuka daraja.” alisema Kapana.

Wakati huohuo rafiki wa karibu wa Mwanuke amefichua kuwa beki huyo amejiunga na Mtibwa kwa mkopo akitokea Simba.

“Mwanuke ametolewa kwa mkopo na Simba ili aweze kuisaidia Mtibwa kukwepa janga la kushuka daraja kutokana na kuwa katika nafasi mbaya,” kilisema chanzo.

KUELEKEA MECHI YA LIGI NA AZAM FC…MASTAA SIMBA WAPEWA ‘HONEY MOON’ YA SIKU 10… PHIRI, BALEKE ‘WAWEKEWA PANGA SHINGONI’…BENCHEKH AWAKATAA HADHARANI…MANGUNGO ATIA NENO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply