FT:Simba 1-0 Jamhuri
Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA LIGI NA AZAM FC…MASTAA SIMBA WAPEWA ‘HONEY MOON’ YA SIKU 10…

admin January 15, 2024 8:22 pm

KOCHA wa Simba, Abdelhak Benchikha wamewapa mapumziko ya siku 10 wachezaji wake ambapo watarejea kambini Januari 24 mwaka huu, kujiandaa na mechi mbalimbali za mashindano wanayoshiriki.

Mapumziko ya wachezaji hao yameanza mara baada ya kurejea kutoka kisiwani Zanzibar, ambako timu hiyo ilikuwa inashiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Katika mashindano hayo, Simba ilikuwa mshindi wa pili huku Mlandege ikitetea kombe hilo kwa ushindi wa bao 1-0, mchezo uliochezwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Amaan Complex, Unguja.

Simba ikirudi kambini itakuwa na kibarua cha kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi pamoja na mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Miongoni mwa mechi ambazo huenda Simba ikaanza nazo ligi itakaporejea baada ya kumalizika kwa michuano ya Afcon inayoendelea nchini Ivory Coast ni zile za viporo dhidi ya Azam FC, Mashujaa na Geita Gold FC.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema wachezaji wamepewa mapumziko kwa siku hizo kwani wamekuwa katika majukumu ya timu kwa muda mrefu.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola amesema kuwa; “Kila mchezaji amepewa programu yake ambapo kocha mkuu atakuwa anafuatilia, maana hawawezi kukaa hivi hivi kwa siku zote hizo.”

KUHUSU ISHU YA CAF KUFUTA KOMBE LA SHIRIKISHO…MAPYA HAYA HAPA… MASTAA WALIOPIGWA PANGA SIMBA KUPETA NA TIMU HIZI ZA LIGI KUU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply