Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO….LWANGA NA AKPAN KUPISHANA MSIMBAZI…MCHORO MZIMA UKO HIVI…

KUELEKEA MSIMU UJAO….LWANGA NA AKPAN KUPISHANA MSIMBAZI…MCHORO MZIMA UKO HIVI…


Imethibitishwa kuwa kiungo mkabaji kutoka Uganda, Taddeo Lwanga ataondoka Msimbazi ili kumpisha Mnigeria, Victor Akpan anayekipiga Coastal Union.

Akpan amesainishwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo, huku akisubiri kumaliza kibarua chake akiwa na Coastal katika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itakayopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa mabosi wa klabu hiyo wamekubaliana kuachana na Lwanga kwa kumtoa kwa mkopo kwani mkataba wake umebaki mwaka mmoja na nusu na si rahisi kuuvunja kwani gharama itakuwa kubwa zaidi.

Viongozi hao wa Simba wameanza mchakato wa kumtafutia timu Lwanga ili wamtoe kwa mkopo na wameamua kufanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake msimu huu tangu alipotoka kwenye majeraha.

Inaelezwa viongozi wa Simba wamefikia uamuzi huo kwa sababu hawawezi kuwa na wachezaji wawili wanaocheza nafasi moja ya kiungo mkabaji na waliamua kumsajili Akpan kuongeza uimara wa eneo la kiungo wa ukabaji kutokana na Lwanga kushindwa kuwa kwenye ubora wake msimu huu.

“Ishu ya Akpan imeshakamilika, ila hajalipwa chake kwani wanasubiri amalize kuitumikia Coastal katika fainali ya ASFC, kisha klabu yake itoe barua ya kumuachia, atapishana na Lwanga ambaye anatolewa kwa mkopo,” kilisema chanzo chetu makini ndani ya Simba.

SOMA NA HII  KIPA LA SIMBA 'LAJITIA KITANZI' MBEYA CITY...ISHU NZIMA IKO HIVI....