Home Habari za michezo ACHANA NA YANGA KUWA BINGWA MSIMU HUU…MSHERY NAYE KAWEKA REKODI HII YA...

ACHANA NA YANGA KUWA BINGWA MSIMU HUU…MSHERY NAYE KAWEKA REKODI HII YA KIPEKEE JANGWANI….


Achana na rekodi ya kutwaa taji ndani ya nusu msimu tangu aliposajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar hapa namzungumzia kipa Abutwalib Mshery ambaye ameweka rekodi mbili ndani ya timu hiyo.

Mshery amesajiliwa na Yanga dirisha dogo la usajili na tayari amecheza mechi saba ndani ya timu hiyo akiruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja tu.

Ukiachana na hilo kipa huyo namba mbili wa Yanga amevunja rekodi ya kuwa mwiba kwa Coastal Union kutokana na kucheza mechi tatu dhidi yao akiwa langoni na hajaruhusu nyavu zake zitikiswe.

Kipa huyo chipukizi anayeichezea pia timu ya taifa, Taifa Stars ametumia dakika 270 dhidi ya Coastal akiwa na timu mbili tofauti bila kuruhusu bao.

Mshery alianza kukaa langoni dhidi ya Coastal akiwa na timu yake ya zamani Mtibwa Sugar wakiibuka na ushindi wa bao 1-0, mechi iliyopigwa Mkwakwani mwishoni mwa mwaka jana kabla ya kusajiliwa na Yanga na kuidakia katika mechi mbili na zote Yanga imeshinda.

Mechi ya kwanza ilikuwa ni ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Coastal Union ugenini Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na juzi tena alisimama langoni Yanga ikitawazwa mabingwa baada ya ushindi wa mabao 3-0.

Hadi sasa kipa huyo amecheza michezo 18 kwenye Ligi Kuu Bara kati ya hiyo 11 alikuwa Mtibwa Sugar na saba Yanga ameweka rekodi ya nyavu zake kutokutikiswa mara 10 kati ya michezo hiyo.

Akizungumza Mshery alisema; “Kwanza nina furaha kubwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango kwenye timu hadi inatwaa kombe la Ligi Kuu Bara mengine ni sehemu ya majukumu na malengo yangu mimi kama mchezaji.”

“Ubora wa kikosi kuanzia washambuliaji hadi mimi kama mlinda mlango ndio siri ya mafanikio haya yaliyotoa furaha kuanzia viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na watanzania wote wanaoipenda Yanga.”

SOMA NA HII  MASTAA IMBA ATOA AHADI YA KIBABE DHIDI YA WYDAD LEO