Azam FC

AZAM FC WAJIBU MAPIGO KWA SIMBA NA YANGA…WASHUSHA KINDA LA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST..NI BALAA NA NUSU…

admin June 30, 2022 3:38 pm


Klabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Kiungo Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior Kwa mkataba wa miaka mitatu.

Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel, amenunuliwa na Azam FC kutokea timu ya Sol FC ya kwao,Na pichani akisaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa (@yusufbakhresa) na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin (@abdulkarim.amin).

Nyota huyo aliyekuwemo kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017-2018.

Kiungo huyo mshambuliaji, 22, mwenye kipaji cha hali ya juu pia aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas, 2018-2020.

Ubora wake ulimfanya pia kuchezea timu za Taifa za vijana za Ivory Coast U-15 na U-17, pamoja na kikosi cha wachezaji wa ndani (CHAN) 2020.

KISA PAPE SAKHO…LUIS MIQUISSONE ATAJWA TENA SIMBA….TATIZO LAKE LAWEKWA WAZI… KWA KAULI HII YA AJABU YA MWAKALEBELA KUHUSU CAF…INADHIHIRA MAWAZO NA MITAZAMO YA YANGA KWA UJUMLA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply