Home Azam FC AZAM WAIONYESHA SIMBA JEURI YA PESA….WATUMIA MAMILIONI KUWAPORA ‘BEKI LA KAZI’…

AZAM WAIONYESHA SIMBA JEURI YA PESA….WATUMIA MAMILIONI KUWAPORA ‘BEKI LA KAZI’…


SIMBA inataka kujipanga upya kwa kusajili majembe ya maana, lakini wakati ikitafakari namna ilivyojikwaa hadi kutema mataji yake yote mawili makubwa, imepigwa kanzu katika mbio za kuiwania saini ya beki wa Ruvu Shooting, Nathaniel Chilambo.

Chilambo alikuwa miongoni mwa majina yaliyopendekezwa kwenye usajili wa Simba lakini Azam nao walishavutiwa na ubora wa nyota huyo na kuchangamka fasta kuinasa saini yake.

Imeelezwa kuwa mazungumzo ya mabosi wa Simba na Chilambo yalikwenda mbali zaidi hadi kukubaliana kiasi cha Sh 30 milioni ambacho mchezaji angechukua kama dau la usajili na mshahara kwa mwezi ungekuwa Sh 2 milioni.

Inafahamika wakati Simba wakiishia hapo matajiri wa Azam FC wameingilia kati dili hilo na kumsainisha mkataba wa awali (pre contract) beki huyo kimya kimya huku wakimuahidi zaidi maslahi mazuri yaliyomvutia Chilambo.

Baada ya mazungumzo yenye usiri mkubwa, Chilambo alikubali kusaini mkataba wa awali wa mwaka mmoja wa matajiri hao.

Azam inahitaji beki wa kulia kutokana na waliopo sasa, Nicolas Wadada na Abdul Hamahama hawatumiki hivyo nafasi hiyo kucheza Lusajo Mwaikenda ambaye ni beki wa kati au Paul Katema ambaye ni kiungo mkabaji.

SOMA NA HII  KISA YANGA KUKUTANA NA WASAUZI...ABDI BANDA AIBUKA NA HILI JIPYA...'AMFUNDISHA KAZI' NABI...