Home Uncategorized JEMBE LA YANGA MAMBO SAFI

JEMBE LA YANGA MAMBO SAFI

 


BAADA ya kuenea kwa tetesi nyingi juu ya usajili wa straika mpya wa Yanga, raia wa Congo, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Angers ya Ufaransa, Ferebory Dore, anayetajwa kama pacha wa Said Ntibanzokiza ‘Saido’ anatarajia kutua nchini na kujumuika na kikosi hicho tayari kwa kuanza kazi.

 

Tayari Yanga wanadaiwa kumalizana na Dore kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said ambaye tayari ameshamaliza biashara na vibali vya mchezaji huyo, Dore mwenye umri wa miaka 31, akitokea Brazzaville, Congo.

 

Dore hadi anaingia rada za Yanga ni mchezaji huru pamoja na huko nyuma kuwahi kukipiga katika Klabu ya Angers ya Ufaransa.

 

Chanzo chetu makini kimeeleza kuwa, tayari Hersi amemaliza dili hilo na muda wowote kuanzia sasa ataanza kuchapa kazi hiyo hivi karibuni.


Kwa sasa kila kitu kuhusiana na mchezaji huyo kimekamilika na kitu kikubwa ambacho kinasubiriwa ni muda tu wa kutambulishwa nyota huyo.

 

“Viongozi tayari wamemaliza kila kitu kuhusiana na vibali vyake na sasa ni yeye tu kujumuika na wenzake kwa ajili na kuanza kucheza,” kilisema chanzo hicho.

 

Hivi karibuni Injinia Hersi aliweka wazi kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na mchezaji ambaye atakuja kuingia moja kwa moja kikosini jambo ambalo sasa limeanza kujidhihilisha kutokana na taarifa hizi.

 

Chanzo:Championi

SOMA NA HII  VIDEO: BAADA YA KUWATUNGUA SIMBA NA YANGA, MTUPIAJI ILANFYA AWEKWA KWENYE RADA ZAO