Home Habari za michezo YANGA KWENYE KIBARUA KIGUMU

YANGA KWENYE KIBARUA KIGUMU

Habari za Yanga

YANGA kesho  ina kibarua kigumu kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mchezo huo utakaochezwa saa 1:00 usiku Yanga watakuwa wenyeji kusaka alama tatu za nyumbani baada kupoteza mechi ya kwanza na CR Belouizdad ya Algeria na kuwakaribisha Al Ahly kwa kusaka alama tatu muhimu .

Wakati Yanga ikidhamilia kucheza damu na jasho huku Al Ahly  mechi yao kwanza walishinda 3-0  dhidi ya Medeama ya Ghana , mchezo uliopigwa nchini Misri

Yanga na Al Ahly wamekutana mara sita, Yanga wameshinda moja sare moja na kupoteza michezo minne, Waaarabu hao walishindwa michezo na ushindi mkubwa kwa timu hiyo dhidi ya Yanga 2-1 , 2016, nchini Misri.

Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema wamejiandaa vizuri wamepata muda wa kupumzika kwa wachezaji wake waliotoka katika majukumu ya Taifq.

Amesema  maandalizi waliyoyafanya kuelekea mchezo wa leo kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri na kuweza kuvuna alama tatu muhimu katika mchezo wa nyumbani.

“Wachezaji wana morali kwa mchezo huo, Al Ahly , timu kubwa kwa Afrika lakini tunaenda kucheza 11 na wao 11 hivyo tunaenda kukutana nao use kwa uso kila kitu kinawezakana ndani ya dakika 90.

Tulipoteza mechi nchini Algeria tukarudi nyumbani na kufanyia kazi madhaifu yetu na tunaenda kukutana na timu ambayo inafalssafa ya timu ambayo tumetoka kucheza nao CR Belouizdad,  lakini huu muda  haturuhusu kufanya makosa yaliyojitokeza awali,” amesema Gamondi .

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema wamejipanga vizuri na wamesahau matokeo yaliyopita na sasa wanampango mzuri wa kutafuta ushindi nyumbani.

Amesema wameangalia ubora wa safu ya ushambuliaji kama beki wamejipanga vizuri kutoruhusu washambuliaji na kazi iliyopo kwa viungo wao na washambuliaji kufanya majukumu yao.

“Tumejipanga vizuri na tuko tayari kukutana na Al Ahly, tunatambua utakuwa mchezo mgumu lakini tumedhamilia kupambana kutafuta ushindi katika mchezo wetu wa nyumbani,” amesema Mwamnyeto.

Kocha Mkuu wa Al Ahly, Marcel Koller  amesema  wako tayari kucheza mechi hiyo ambayo ni timu ngumu kulingana na matokeo ya mechi iliyopoita haitakuwa mechi rahisi kwa sababu ya wapinzani wao kupoteza na wako nyumbani.

Amesema haangalie historia ya Yanga kikubwa wanaangalia mechi iliyopo mbele yao na maandalizi waluyoyafanya kwa kutafuta pointi tatu muhimu kwenye mchezo ambao wanacheza ugenini.

“Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu kila mmoja wetu anahitaji matokeo, hatukuwa na matokeo mazuri ndani ya uwanja huu lakini kila siku kuna vitu vipya na maandalizi kulingana na mechi tunayokwenda

Kila siku kuna kitu kipya ni hatukuweza kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja huu lakini tumejiandaa vizuri na kuhakikisha tunashinda katika mchezo wetu wa kesho (leo),” amesema Koller

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA YANGA NA SIMBA ZILIVYOCHEZA JANA....KMC WAJIPIGAPIGA KIFUANI NAKUUTAKA UBINGWA WA LIGI..