Home Habari za michezo BAADA YA KUPEWA ‘UKOCHA MKUU’ KWA MUDA….HIZO TAMBO ZA MATOLA KWA MBEYA...

BAADA YA KUPEWA ‘UKOCHA MKUU’ KWA MUDA….HIZO TAMBO ZA MATOLA KWA MBEYA CITY UTAFIKIRI MOURINHO AISEE…


Kikosi cha Simba juzi kilicheza mechi ya kirafiki na Kituo cha Cambiaso kwa lengo la kunoa makali yao kabla ya kuvaana na Mbeya City, huku kaimu kocha mkuu, Seleman Matola akitamba kwamba licha ya kuelekea kupoteza ubingwa, lakini kazi haijaisha katika Ligi Kuu Bara.

Matola anayekaimu ukocha mkuu baada ya aliyekuwa bosi wake, Pablo Franco kutimuliwa alisema wanajua ishu ya ubingwa kwao imeshafeli, lakini kwa vile ligi haijamalizika na ndio maana anaendelea kuwafua vijana wake ili wahakikishe wanamalizia mechi tano zilizosalia kibabe.

Akizungumza juzi mara baada ya mazoezi ya asubuhi, Matola alisema wanajua wana mechi tano za kukamilisha msimu, huku watani wao Yanga wakionekana wakiwa na nafasi kubwa ya kubeba ubingwa, lakini hawajaridhika eti wamalize ligi kinyonge.

“Ni kweli kwenye ubingwa tumeshasamehe, lakini hatutakubali kumaliza kinyonge mechi zilizosalia, tunaendelea kujifua ili kupata ushindi tukianza na Mbeya City ambao walitufunga katika pambano la awali ugenini,” alisema Matola.

Simba ilitunguliwa bao 1-0 na Mbeya City, ikiwa ni kati ya mechi mbili ilizopoteza ikiwamo ya Kagera Sugar, huku ikiwa nafasi ya pili kwa sasa ikikusanya pointi 51 kutokana na mechi 25 nyuma ya Yanga yenye alama 64. Yanga inahitaji pointi tatu katika mechi nne ilizonazo ili kutangaza ubingwa iliyousotea kwa misimu minne mfululizo mbele ya watani wao, Simba.

Mbali na mechi ya Mbeya City inayopigwa Alhamisi hii, Simba ina michezo mingine minne dhidi ya KMC, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Mbeya Kwanza na kama itashinda zote itakusanya jumla ya pointi 15 na kujihakikisha mamilioni ya mshindi wa pili kutoka kwa wadhamini wa ligi.

Mshindi wa pili wa Ligi Kuu anavuna Sh 250 milioni kutoka Azam TV na Sh 50 milioni kutoka NBC walio wadhamini wakuu wa ligi hiyo.

Matola alisema kurejea kwa wachezaji waliokuwa timu za taifa zimesaidia kumrahisishia kazi katika maandalizi ya mchezo wa Mbeya City na mingine ijayo.

SOMA NA HII  YANGA YATUMIA MFUMO WA HISPANIA...AISEE!! KUMBE WALISAINI MKATABA HUU