Home Habari za michezo BINGWA NBC PREMIER LEAGUE KULAMBA MILIONI 600…KOMBE JIPYA LATAMBULISHWA…YANGA WATAKAA NALO SIKU...

BINGWA NBC PREMIER LEAGUE KULAMBA MILIONI 600…KOMBE JIPYA LATAMBULISHWA…YANGA WATAKAA NALO SIKU 30 TU…


Bodi ya Ligi imetaja kitita cha Sh 1.8 Bilioni kama zawadi na bonusi kwenye Ligi msimu huu huku bingwa akitengewa Sh 100 milioni kutoka NBC na Sh 500 Milioni kutoka Azam.

Ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kassongo amebainisha hayo leo wakati wa kutambulisha kombe atakalokabidhiwa bingwa wa msimu huu.

Amesema mshindi wa pili ataondoka na Sh50 milioni kutoka NBC na Sh250 milioni kutoka Azam.

“Watatu atazawadiwa Sh30 milioni kutoka kwa mdhamini wa Ligi, lakini pia 225 kutoka Azam,” amesema.

Katika zawadi hizo, NBC imetenga Sh20 milioni kwenye zawadi ya timu yenye nidhamu.

Kuhusu kombe, Kassongo amesema muonekano wa kombe la ligi utakuwa wa kombe lililotambulishwa leo hadi pale itakavyoamuliwa vinginevyo.

“Bingwa atakaa nalo mwezi mmoja na kulirejesha endapo atalitetea mara tatu ndipo atalichukua moja kwa moja,”

SOMA NA HII  SAKATA LA MORRISON YANGA....NABI AKOLEZA CHUMVI....KAMKATAA MCHANA KWEUPEEE....