Home CAF KISA CAF…IBENGE, MOSIMANE WARUDI RASMI DARASANI UPYAA….KOCHA WA MANE NAYE NDANI…THIERRY HENRY...

KISA CAF…IBENGE, MOSIMANE WARUDI RASMI DARASANI UPYAA….KOCHA WA MANE NAYE NDANI…THIERRY HENRY APEWA SHAVU…


Kocha mkuu wa Al ahly Pitso Mosimane pamoja na Kocha wa Rs Barkane Florent Ibenge ni miongoni mwa makocha 26 niwalioalikwa kuhudhuria kozi ya kwanza kabisa ya CAF Pro leseni – cheti cha juu zaidi cha ukocha barani Afrika.

Mosimane mwenye makombe matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ibenge aliyetoka kutwaa Kombe la Shirikisho la Afrika msimu huu wameungana na makocha wengine akiwemo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal Aliou Cissé alitwaa taji la AFCON 2021.

Ukiachana na Makocha hao watatu wengine 23 waliobaki ni kutoka Morroco akiwemo na Kocha wa Wydad Casablaca Walid Regragui ambaye ambaye ametoka kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Kozi hiyo imeonekana kuendeshwa kwa namna tofauti  huku mara nyingi makocha hao wameonekana wakipatiwa mafunzo wa wakufunzi wao kwa njia ya mtandao ambapo hili lilithibitishwa baada ya Kocha Mosimane kutupia picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ikimuonyesha yeye na Mchezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry wakizungumza kwa njia ya ‘Video call’

Shirikisho la soka la Afrika CAF limekuja na kozi hii kwa lengo la kuongeza utaalamu ili makocha wa ndani waweze kuzingatiwa katika mfumo wa ikolojia, haswa na wenzao kutoka mabara mengine.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUWAACHA KONKONI , GIFT....MABOSI YANGA WAPASUA VICHWA...