Home Uncategorized SAMATTA: KESHO TAIFA NI MWENDO WA BURUDANI, MASHABIKI JITOKEZINI KWA WINGI

SAMATTA: KESHO TAIFA NI MWENDO WA BURUDANI, MASHABIKI JITOKEZINI KWA WINGI

NAHODHA wa timu ya Taifa, Mbwana Samatta amesema kuwa mashabiki kesho wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa kutoa sapoti kwenye mchezo wa hisani dhidi ya timu ya Ali Kiba utakaochezwa majira ya saa 10:00 Jioni.

Akizungumza na SalehJembe, Samatta amesema kuwa wakati sahihi wa kujitoa kwa ajili ya jamii ni sasa hivyo wao wanaanza wengine watafuata.

“Ni mradi ambao upo kwa ajili ya jamii yetu, tunajua kwamba uhitaji ni mkubwa ila ni mwanzo mzuri, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna tutakavyowapa burudani na pia tunarejesha kile tunachokipata kwa jamii,” amesema Samatta.

Mradi wa Samata na Kiba umepewa jina la SAMAKIBA Foundation na ulianza mwaka jana ambapo walirejesha kwa wanafunzi wanaoshi kwenye mazingira magumu, msimu huu ni mara ya pili.

SOMA NA HII  WANYAMA AMKARIBISHA SAMATTA UINGEREZA