Home Habari za michezo KAMPENI YA KUJENGA UWANJA…SIMBA WAANIKA WAZI WALICHOKIAMBULIA KWA MASHABIKI…AHMED ALLY AGUNA…

KAMPENI YA KUJENGA UWANJA…SIMBA WAANIKA WAZI WALICHOKIAMBULIA KWA MASHABIKI…AHMED ALLY AGUNA…


Hatimaye Simba imeweka wazi amendeleo ya michango yao juu ya kampeni za ujenzi wa uwanja wao.

Meneja mawasiliano wa Simba, Ahmedi Ally amesema mpaka sasa kupitia kampeni yao ya Tumeanza na tunaweza mashabiki na wanachama wao wamechangia kiasi cha Sh 60 milioni.

Ahmedi amesema fedha hizo bado ziko salama katika malengo yaliyokasudiwa na uongozi wa klabu hiyo.

Aidha Ahmedi amekiri kwamba bado muitikio wa michango hiyo licha ya kuanza kwa kasi bado haitaweza kufikisha malengo yao.

“Michango hii iko salama na tunawashukuru wanachama na mashabiki ambao wameendelea kuchanga,hakuna pesa ambayo itakwenda kutumika kwenye malengo tofauti,amesema Ahmedi.

“Hatuwezi kusema hizi Sh60 milioni tunaweza kujenga uwanja, safari bado ndefu lakini sasa bado tunataka nguvu zaidi ya michango ya Wanasimba,”

SOMA NA HII  ISHU YA MEDDIE KAGERE KUSEPA SIMBA IPO HIVI