Home Simba SC AZAM WAMETUKUMBUSHA MAPUNGUFU YETU

AZAM WAMETUKUMBUSHA MAPUNGUFU YETU

 


KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amesema kuwa mchezo uliopita dhidi ya Azam umewasaidia kujua mapungufu waliyonayo na kuyafanyia kazi kabla ya kuivaa AS Vita.

Juzi Jumapili Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam katika mchezo mkali wa kiporo cha Ligi Kuu Bara uliopigwa katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba imeondoka nchini leo kuelekea DR Congo kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa kundi A, hatua ya makundi, Ligi ya mabingwa Afrika utakaopigwa siku ya Ijumaa.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka nchini Gomes amesema: “Kwenye mchezo dhidi ya Azam tuliacha eneo kubwa wazi na kuwafanya wapinzani wetu watushambulie zaidi.

“Lakini pia tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga ambazo tulishindwa kuzitumia, hivyo kuelekea mchezo huu dhidi ya AS Vita tumerekebisha makosa hayo na nina imani kubwa makosa hayo hatutayarudia,”

SOMA NA HII  CHAMA AIVURUGA SIMBA, MO AIBUKA