Home news BAADA YA KUMALIZA KIFUNGO CHA TFF…PABLO AIVUA UBINGWA SIMBA…AGUSIA TIMU YAKE INAVYOCHEZA…

BAADA YA KUMALIZA KIFUNGO CHA TFF…PABLO AIVUA UBINGWA SIMBA…AGUSIA TIMU YAKE INAVYOCHEZA…


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco raia wa Hispania, amefunguka kuwa anaamini ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu hauna mwenyewe, licha ya wapinzani wao Yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano.

Pablo ametoa kauli hiyo baada ya juzi Jumapili Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza na kufikisha pointi 31 ikiwa ni tofauti ya pointi tano dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Yanga wenye pointi 36.

Akizungumza na Soka la Bongo, Pablo alisema kupata matokeo hayo ya ushindi kumerudisha hali ya kuendelea kufanya vizuri katika mechi za ligi licha ya kukiri kuwa bado suala la ubingwa mpaka sasa halina mwenyewe kutokana na ushindani ulivyo.

“Hatukuwa kwenye kipindi kizuri, lakini tumeanza kurejea taratibu kwa kupunguza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wetu, kwetu ni jambo zuri kwa kuwa tumerejea katika malengo yetu japokuwa bado tunatakiwa kupambana zaidi kwa kuhakikisha timu inapata matokeo makubwa.

“Kuhusu suala la ubingwa ndiyo malengo yetu makubwa ingawa bado kwa sasa upo wazi kwa timu zote zinaweza kufanya maajabu kwani timu zina mechi nyingi, lakini kitu ambacho tunaendelea kukiangalia zaidi upande wetu ni kuhakikisha tunaendelea kupata matokeo makubwa ili kufika tunapotaka,” alisema Pablo.

SOMA NA HII  YANGA YATUMA SALAMU GEITA GOLD