Home Uncategorized MOURINHO:NILIWAHESHIMU WAPINZANI

MOURINHO:NILIWAHESHIMU WAPINZANI


KOCHA Mkuu wa Tottenham Hotspurs, Jose Mourinho amesema kuwa siri kubwa ya kushinda kwenye mchezo wao dhidi ya Brentford ni kuwaheshimu wapinzani wake.

Mourinho amesema:”Nimekuja England 2004 na kumbuka kwamba wakati huo ilikuwa ni lazima kwangu kujifunza katika jambo ambalo ninafanya lazima niwe na nidhamu.

“Ikiwa kuna siri yoyote ambayo nimechukua na kuifanyia kazi ni kuheshimu timu ambazo zipo ndani ya England pamoja na wapinzani wangu bila kujali hiyo timu inashiriki ligi ipi na wakati gani. Kuna timu ambazo huwa zinashangaza baada ya mchezo kwa kupata matokeo ambayo yanashangaza pia,”.

Nyota wa Tottenham Hotspur, Moussa Sissoko dakika ya 12 na Son Heung-min dakika ya 70 walipeleka maumivu kwa Brentford waliomaliza pungufu baada ya Josh Dasilva kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 84, Uwanja wa Tottenham Hotspur.

Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali unaifanya Spurs kutinga hatua ya fainali ikiwa ni ya kwanza kwa Kocha Mkuu, Jose Mourinho baada ya kujiunga na kikosi hicho Novemba 20.

Mourinho aliibuka ndani ya Spurs mwaka 2020 akichukua mikoba ya Mauricio Pochettino ambaye alifutwa kazi ndani ya kikosi hicho na kwa sasa amepata dili ndani ya PSG.


Fainali yake kwenye Kombe la Carabao itakuwa ni dhidi ya Manchester United ama Manchester City ambao wanacheza leo hatua ya nusu fainali.
SOMA NA HII  VIDEO:HIVI NDIVYO VIPIMO AMBAVYO WAMEFANYA YANGA