Home news PAMOJA NA YOTE YALIYOMPATA..NYOTA YA KABWILI YAZIDI KUNG’AA…AISAIDIA TIMU YAKE KUSHINDA NG’OMBE…

PAMOJA NA YOTE YALIYOMPATA..NYOTA YA KABWILI YAZIDI KUNG’AA…AISAIDIA TIMU YAKE KUSHINDA NG’OMBE…

BAADA ya kutoonekana ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu, golikipa Ramadhan Kabwili, ameonekana akicheza fainali ya Kombe la Ng’ombe akiwa na Tabata FC.

Kabwili ambaye aliondoka kambini tangu Yanga ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo uliochezwa Novemba 20, 2021, mpaka leo hajaonekana akiwa na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Juzi Jumapili, Gazeti la Spoti Xtra lilimshuhudia kipa huyo akiwa kwenye kikosi cha Tabata FC ambacho kilicheza mchezo wa fainali ya kombe la Ng’ombe dhidi ya Tabata Future kwenye Uwanja wa Tabata Shule uliopo Tabata jiji Dar.

Mchezo huo ulimalizika kwa Tabata FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuchukua zawadi ya ng’ombe huku Tabata Future wakiambulia mbuzi wawili ambao ni zawadi ya mshindi wa pili.

SOMA NA HII  BEKI SIMBA ATUMIWA FEDHA ZA KUMZUIA MAYELE...ORLANDO WAUHOFIA MZIKI WA SIMBA...| SpotiXtra...