Home Uncategorized TANZANITE YABEBA KOMBE LA COSAFA, YALIPA KISASI KWA ZAMBIA LEO

TANZANITE YABEBA KOMBE LA COSAFA, YALIPA KISASI KWA ZAMBIA LEO

TIMU ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ leo imetwaa ubingwa wa michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini baada ya kulipa kisasi mbele ya Zambia.

Tanzanite iliyo chini ya Kocha Mkuu Bakari Shime kwenye hatua ya makundi ilipokutana na Zambia ilifungwa mabao 2-1 na leo wamerejesha mabao na kusepa na kombe lao licha ya kualikwa kwenye michuano hiyo.

Mabao kwa upande wa Tanzanite yalipachikwa na Opa Clement dakika ya 24 pamoja na Protasia Mbunda aliyefunga dakika ya 87 Uwanja wa Wolfson Port Elizabeth.

SOMA NA HII  BALINYA AMTIKISA KAGERE BONGO