Home Habari za michezo CHAMA AIVURUGA SIMBA, MO AIBUKA

CHAMA AIVURUGA SIMBA, MO AIBUKA

Habari za Simba SC

WAKATI nyota wanne wa Simba wakisafiri jana alfajiri kwenda kambini nchini Uturuki, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mzambia, Clatous Chama amebaki Dar, huku sakata lake la mkataba likishughulikiwa na uongozi wa juu akiwemo Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’.

Kikosi cha Simba kipo kambini Uturuki tangu wiki iliyopita kikijiandaa na msimu ujao ambao timu hiyo imeweka malengo ya kuchukua makombe yote ya ndani na kufika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’.
Simba ikiwa kambini huko Uturuki, Chama ameonekana kugomea kwenda, hadi pale atakapoboreshwa baadhi ya makubaliano yaliyokuwepo katika mkataba wake ikiwemo mshahara.

Akizungumza , Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa kundi la pili la wachezaji wanne jana alfajiri lilisafiri kwenda Ankara, Uturuki kwa ajili ya kuungana na wenzao kambini.

Ally aliwataja wachezaji hao ni Aubin Kramo, Willy Onana, Che Malone Fondoh ambao ni wapya, sambamba na Jean Baleke.

Aliongeza kuwa, Chama bado hajaondoka na suala lake lipo kwa viongozi wa juu wakijaribu kulishughulikia, watakapokamilisha ataungana na wenzake.

“Chama hajaondoka na suala lake lipo kwa viongozi wa juu wakijaribu kilishughulikia, litakapoisha tutawajulisha, lakini ifahamike Chama hayupo kwenye safari hii ya kundi la pili la wachezaji walioelekea Uturuki leo (jana) Jumatatu.

“Wachezaji waliosafiri ni Kramo, Onana, Fondoh na Baleke ambao wanakwenda kuinogesha kambi yetu iliyokuwepo huko Uturuki ambayo inafikisha wiki ya pili,” alisema Ally.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAKE WAPYA, ROBERTINHO AWAPIGA MKWARA MZITO YANGA