Home Habari za michezo BAADA YA SIMBA KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAKE WAPYA, ROBERTINHO AWAPIGA MKWARA MZITO YANGA

BAADA YA SIMBA KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAKE WAPYA, ROBERTINHO AWAPIGA MKWARA MZITO YANGA

Habari za Simba SC

SIMBA jana iliendelea kuwapa raha mashabiki wake kwa kutambulisha chuma kingine kipya, huku kocha mkuu wa timu hiyo aliyerejea juzi mchana akisema kwa majembe yaliyosajiliwa kikosi sasa kimebalanzi na kuzipiga mkwara timu pinzani akisema; “Tukutane uwanjani muone”.

Kocha huyo Mbrazili alisema amekoshwa sana na namna mabosi wa Simba walivyotekeleza mapendekezo yako kwenye usajili kwani umeifanya timu hiyo ienee kila idara kwa sasa na kumpa jeuri ya kuamini atasumbua sana kwenye msimu ujao mbele ya wapinzani wao hasa Simba na Azam.

Robertinho alizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege, alisema kwa kujiamini kuwa kwa usajili ambao umefanywa, ni wazi heshima ya klabu hiyo inarudi tena baada ya kumaliza misimu miwili mfululizo bila kutwaa taji lolote mbele ya Yanga.

Simba imeshawatangaza mawinga wawili wapya, Leandre Onana kutoka Rayon Sports ya Rwanda na Aubin Krabo aliyekuwa Asec Mimosas ya Ivory Coast najana imemtambulisha beki wa kati, Che Fondoh Malone kutoka CotonSport ya Cameroon.

Mbali na hao pia Simba inahusishwa kumalizana na mshambuliaji Fabrice Ngoma aliyekuwa Al Hilal ya Sudan sambamba na kipa Mbrazili, Caique Luiz Santos anayetua kati ya leo na kesho kabla ya Jumanne timu kusepa kwenda kambini ya maandalizi ya msimu huko Uturuki.

Mbali na nyota hao wapya, lakini Simba imebakiza baadhi ya majembe yake ya kikosi cha kwanza na ilikuwa inamalizana na wachezaji kadhaa wazawa wa kuchukua nafasi za waliotemwa hivi karibuni akiwamo, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, kipa Beno Kakolanya, Habib Kyombo aliyetolewa kwa mkopo Singida Big Stars sambamba na Mkenya Joash Onyango.
Kutokana na hilo kocha Robertinho alisema kilichotokea msimu uliopita wamekifanya chachu ya kuona kwa namna gani wanaweza kurejea msimu ujao wakiwa bora zaidi, hivyo iliwabidi kuingia sokoni na kusaka vifaa vya maana.

“Kuifanya Simba kuwa mbali kiushindani na klabu zote kwenye ligi ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu, tunataka kutengeneza gepu kubwa kati yetu na wao ndio maana tumesajili wachezaji ambao wataongeza upana na ubora kwenye kikosi chetu,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Ufinyu wa kikosi msimu uliopita ulikuwa ukituumiza, tulikuwa na michezo ambayo tulihitaji mabadiliko lakini utofauti wa ubora wa wachezaji ulitufanya kushindwa kupata tulichotaka.”
Kocha huyo aliongeza kwa kusema; “Ninayo furaha na utambulisho wa wachezaji, kwani nilikuwa najulishwa kila kilichokuwa kikifanyika, viongozi wamefanya kazi kubwa sasa ni wakati wetu wa kujiandaa na kutafuta uwiano mzuri wa uchezaji kama timu.”

Nyota wa kigeni waliosajiliwa wanakuja kuziba nafasi zilizoachwa na Augustine Okrah, Nelson Okwa, Victor Akpan, Mohamed Ouattara, Ismael Sawadogo na Joash Onyango ambao sasa wataungana na Clatous Chama, Henock Inonga, Jean Baleke, Saido Ntibazonkiza, Moses Phiri, Sadio Kanoute pamoja na Pape Ousmane Sakho na Peter Banda ambao nao watajawa kuwa mguu ndani mguu nje kikosini, ili kubalanzi idadi ya nyota wa kigeni (12) wanaotakiwa kikanuni.

SOMA NA HII  MGUNDA: LEO 'TUTAWATEMBEZEA MOTO' USIOZIMIKA POLISI TZ....