Home Habari za michezo KOCHA MPYA WA YANGA AANZA KAZI KIBABE, AWAITA MASTAA WOTE AWAPA NENO...

KOCHA MPYA WA YANGA AANZA KAZI KIBABE, AWAITA MASTAA WOTE AWAPA NENO HILI

Kocha Mpya wa Yanga

KOCHA Mpya wa Yanga Miguel Gamondi tayari yupo nchini kuanza kibarua akiwa ndani ya ardhi ya Tanzania, lakini alipotua tu kauli ya kwanza ikawa ni makombe na soka la maana kwa timu yake, kisha akaenda kupumzika kabla ya leo kupanga kufanya vikao vizito na viongozi wa klabu hiyo.

Gamondi aliotua alfajiri ya kuamkia jana akitokea Hispania na leo atakutana na mabosi wa Yanga akiwemo rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said katika kumalizia hatua za kuunda benchi lake jipya na usajili wa kikosi kwa ajili ya msimu ujao akisisitiza ataendeleza alipoachia mtangulizi wake.

Mwanaspoti lililokuwa la kwanza kuzungumza na kocha huyo mara baada ya kutua jana alfajiri, linafahamu kuwa kikao cha kocha huyo ambaye tayari alishatuma majina ya wasaidizi wake watajadili hatua ya kumalizia mazungumzo na watu hao ambao wanaweza wasipungue wawili.

Kocha huyo amewapa mabosi wake majina ya msaidizi wa kwanza, kocha wa viungo na yule wa makipa ambapo watajadili maamuzi ya mwisho kati hao ikitegemea na uamuzi wa kocha Mrundi Cedric Kaze ambaye alikuwa bado hajatoa jibu la moja kwa moja kama atasalia.

Mapema kocha huyo wakati akiwasili asubuhi alisema yuko tayari kuanza kazi ambapo anajua amekuja kuungana na klabu yenye kiu ya makombe na kwamba hilo litaendelea.
Gamondi alisema katika kipindi ambacho atakuwa Yanga anataka kikosi cha timu hiyo kicheze soka la malengo lakini pia ikicheza soka la kuvutia na kushambulia.

“Nimewahi kuja hapa (Tanzania), lakini kufundisha hii ni mara yangu ya kwanza, nipo tayari sasa kuanza changamoto mpya nikiwa hapa Yanga, bila shaka kuja kwangu hapa ni baada ya kuvutiwa na mradi ambao niliongea na viongozi wa Yanga akiwemo Rais wa klabu (Hersi),” alisema Gamondi.

“Hii ni klabu kubwa sio tu hapa Tanzania bali Afrika kwa ujumla ndio maana tunaona imekuwa na rekodi kubwa ya mataji na kufanya vizuri zaidi Afrika, kuja kwangu hapa ni kuendeleza hayo mafanikio kwa kuchukua mataji na kuona timu inacheza soka la kuvutia lenye malengo.”

CREDIT : Mwanaspoti

SOMA NA HII  KOCHA IHEFU AFUNGUKA KILICHOWAPONZA