Home Azam FC BAADA YA SIMBA SC KUTEMA TONGE ZNZ….AZAM FC WAITUMBULIA MACHO YANGA SC…

BAADA YA SIMBA SC KUTEMA TONGE ZNZ….AZAM FC WAITUMBULIA MACHO YANGA SC…

Habari za Azam FC

Azam FC imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri ambayo imepoteza michezo yote kwenye kundi lao.

Azam FC ipo kundi A na timu ya Malindi iliyomaliza nafasi ya pili kwa kukusanya pointi nne sawa na kinara wa kundi tofauti ni mabao ya kufunga na Jamhuri ambao haina pointi hata moja ikiruhusu nyavu zao kutikiswa mara tano.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Ismail Aziz dakika 33 na mawili walifungwa na Abdal Suleiman ‘Sopu’ kwa mkwaju ya penati akifunga dakika ya 52 na 81.

Azam FC walicheza kwa kujituma zaidi tofauti na mchezo uliopita dhidi ya Malindi wakiambulia sare ya bao 1-1 na ushindi wa leo wamefikisha pointi nne na mabao manne.

Azam atasubiri mshindi wa kesho wa mechi ya Singida Big Stars dhidi ya Yanga.

Sopu ameibuka mchezaji bora kwenye mchezo wa leo kutokana na kuisaidia timu yake kupata nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali huku kiungo fundi wa timu hiyo James Akaminko ameibuka mchezaji bora mwenye nidhamu.

SOMA NA HII  KUTOKANA NA HALI YA YANGA ILIVYO JOB AJA NA KAULI HII KWA WADAU NA MASHABIKI