Home Habari za michezo KUHUSU KLABU ZILIZOBEBA UBINGWA BILA KUFUNGWA…MANARA AIBUKA NA REKODI ZAKE…AIWEKA YANGA MBELE…

KUHUSU KLABU ZILIZOBEBA UBINGWA BILA KUFUNGWA…MANARA AIBUKA NA REKODI ZAKE…AIWEKA YANGA MBELE…


Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Sunday Manara amesema klabu ya Yanga imewahi kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu (3) bila kufungwa lakini taarifa hiyo haiandikwi na waandishi wa habari kwa sababu hawana utamaduni wa kufanya utafiti (Research).

Manara amesema baadhi ya waandishi wamekuwa wakipotosha watu kwa kudai kuwa vilabu viwili tu vya Simba na Azam ndiyo vilivyofanikiwa kuchukua ubingwa huo bila kufungwa huku vikisahau kuwa Yanga nayo imewahi kuchukua mara tatu bila kufungwa katika miaka ya 1968, 1970 pamoja na 1972 enzi hizo Ligi ikichezwa kwa mfumo wa kikanda.

Msemaji huyo amebainisha kuwa kama waandishi wa habari watasema kuwa ni vilabu viwili tu vya Simba na Azam ndivyo vilivyofanikiwa kubeba ubingwa huo bila kufungwa basi vitalazimika kusema kuwa ni kuanzia mwaka 1982 ambapo mfumo wake ulibadilishwa na kuanza kutumika kwa mfumo wa michezo ya nyumbani na ugenini.

Yanga inatarajiwa kuwakabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam majira ya saa kumi jioni.

SOMA NA HII  KANOUTE ATAMBA AFL AWEKA REKODI HII MPAKA SASA