Home CAF KUWANIA KUFUZU AFCON MWAKANI…MANARA ALAMBA SHAVU TIMU YA TAIFA YA BURUNDI…AIKANA YANGA….

KUWANIA KUFUZU AFCON MWAKANI…MANARA ALAMBA SHAVU TIMU YA TAIFA YA BURUNDI…AIKANA YANGA….


TIMU ya Taifa ya Burundi inatarajia kukabiliana na Timu ya Taifa ya Cameroon katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo, Shirikisho la Soka la Burundi kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu Riziki Jacob limeishukuru Tanzania kwa kuikaribisha timu hiyo pamoja na ukarimu walioupata kutoka kwa wadhamini wao Kampuni ya GSM.

Riziki ameanza kwa kuongelea historia ya undugu na ushirikiano baina ya Tanzania na Burundi tangu wakati wa ukoloni ambapo amebainisha kuwa Tanzania na Burundi ni ndugu kwani wamefanikiwa kushirikiana katika Nyanja zote ikiwemo siasa na ukombozi wa nchi zao.

Naye Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara ameteuliwa na Shirikisho la Soka Burundi kuwa mhamasishaji katika tukio hilo muhimu kwa historia ya nchi ya Burundi

Katikati akiongea na waandishi wa habari ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Burundi Riziki Jacob

Akiongea na Waandishi wa Habari Manara amesema anawaomba watanzania pamoja na warundi wote wanaoishi nchini Tanzania wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu ya taifa ya Burundi katika pambano lake dhidi ya Cameroon litakalopigwa siku ya Alhamisi katika dimba la Benjamin Mkapa.

Manara ameongeza kwa kusema mechi hii haina usimba wala uyanga nay eye ametumika kama msemaji wa timu ya Taifa ya Burundi na si Msemaji wa Yanga hivyo ametoa rai kwa watanzania na wapenzi wa soka kwa ujumla kujitokeza kuishangilia timu ya Taifa ya Burundi.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- HATA TUKICHEZA NA TIMU NDOGO LAZIMA TUFUNGWE...MAKOSA YANAJIRUDIA..AMEFUNGUKA HAYA