Home Habari za michezo RASMI…ZIDANE KUPISHANA NA POCHETTINO PSG….AITWA CHAP QATAR KUMALIZANA NA MATAJIRI…

RASMI…ZIDANE KUPISHANA NA POCHETTINO PSG….AITWA CHAP QATAR KUMALIZANA NA MATAJIRI…


KWA mujibu wa taarifa Zinedine Zidane, anukia Paris Saint- Germain, kama mbadala wa Mauricio Pochettino, aliyekalia kuti kavu kwa mujibu wa ripoti.

Taarifa zimetolewa Pochettino yupo mbioni kufukuzwa PSG, baada ya majadiliano ya mabosi kuridhika na mpango huo.

Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, amesafiri hadi Qatar, kukutana na wamiliki wa PSG kabla ya kusaini mkataba wa kuinoa miamba hiyo msimu ujao.

Zidane hakuwa mzigoni tangu alipoondoka Real Madrid, mwisho mwa msimu wa 2021-2022, na kwa mujibu wa taarifa yupo tayari kuanza maisha mapya PSG.

Zidane alionekana katika fainali ya michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya, Real Madrid ilipomenyana na Liverpool uwanja wa Stade de France mwezi uliyopita.

SOMA NA HII  JEMEDARI SAID:- WALIOFANYA USAJILI WA KINA PETER BANDA NA WENZAKE NDIO WALIOPASWA KUFUKUZWA SIMBA...