Home Habar za Usajili Simba SAKATA LA MIQUISSONE KURUDI MSIMBAZI…BOSI MZITO SIMBA AIBUKA NA HILI JIPYA….AFICHUA A-Z...

SAKATA LA MIQUISSONE KURUDI MSIMBAZI…BOSI MZITO SIMBA AIBUKA NA HILI JIPYA….AFICHUA A-Z UKWELI WA MAMBO…


BAADA ya tetesi nyingi kuzagaa za kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Luis Miquissone raia wa Msumbiji kurejea katika timu hiyo, uongozi wa Simba SC umeibuka na kufungukia ishu nzima.

Luis alijiunga na Al Ahly Agosti 26, 2021 kwa mkataba wa miaka minne akitokea Simba baada ya kucheza kwa takribani msimu mmoja na nusu kuanzia Januari 3, 2020. Mkataba wake utaisha 2025.

Kiungo huyo hivi karibuni tetesi nyingi zilimuhusisha kuwa njiani kurejea Simba kwa kile kilichoelezwa klabu yake kupanga kumtoa kwa mkopo baada ya msimu huu kumalizika.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mulamu Nghambi, amesema kuwa, kwa sasa ni ngumu Al Ahly kumtoa kiungo huyo na kurudi Simba.

Nghambi alisema ugumu huo unatokana na kiungo huyo kuwepo katika mipango ya Kocha Mkuu wa Al Ahly, Pitso Mosimane.

“Ngumu kwa sasa kumpata mchezaji anayecheza timu kubwa zilizopo katika Ukanda wa Afrika, hapo nazuzungumzia Al Ahly, Zamalek, Wydad Casablanca, Kaizer Chiefs na nyinginezo.

“Hivi sasa Luis ameanza kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, hivyo ngumu kumpata kirahisi kama watu wanavypofikiria.

“Labda itokee lakini hadi hivi sasa bado hatujapata taarifa rasmi za kiofisi kutoka Al Ahly juu ya Luis kutolewa kwa mkopo,” alisema Nghambi.

SOMA NA HII  KAMA ULIKUWA HUJUI..HII HAPA REKODI MPYA WALIOANDIKA SIMBA ZNZ...RAIS MWINYI ASHIRIKI...