Habari za michezo

BAADA YA MAYELE KUSHINDWA KUTWA KIATU CHA UFUNGAJI BORA..NABI AIBUKA NA HILI KWA MPOLE..

admin July 2, 2022 10:18 am


Kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amempongeza mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu 2021/22.

Mpole ametwaa kiatu cha ufungaji bora baada ya kufunga mabao 17 huku akimzidi mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kwa bao moja ambapo alimaliza na mabao 16.

Nabi amesema wanampongeza Mpole kwa kuibuka kinara wa ufungaji huku akiongeza kuwa Mayele kwa sasa amevunjika moyo kwa kuwa baadhi ya mabao yake mawili yalikataliwa lakini pia muda mrefu ndio alikuwa anaongoza.

Aliweka wazi kuwa anaamini mchezaji huyo ametimiza malengo ya timu kwa maana ya kuipa ubingwa wa ligi na kesho anaenda kuipa tena ubingwa mwingine wa FA dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

YANGA WATAMBA KUIPAPATUA VILIVYO COASTAL UNION LEO…MASHABIKI WAPANGA KWENDA NA ROYAL TOUR.. SIMBA HAWATAKI UTANI AISEEE…WAMALIZANA NA STARIKA HATARI LA MAGOLI KUTOKA UGANDA USIKU USIKU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply