Azam FC

FAGIO LA CHUMA LAZIDI KUPITA NA MASTAA AZAM FC…KIGONYA NAYE ATUPIWA VIRAGO MCHANA MCHANA….

admin July 3, 2022 5:06 pm


UONGOZI wa Azam FC umefikia makubaliano ya pande mbili kwa ajili ya kuvunja mkataba na aliyekuwa kipa wake Mganda, Mathias Kigonya.

Mara baada ya msimu wa 2021/22 kumalizika nyota huyo alibakiza miezi sita kwenye mkataba wake huku akiwaomba viongozi wa kikosi hicho kuomba kuondoka ili akapate changamoto sehemu nyingine msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa na timu hiyo ilieleza kumshukuru Kigonya katika kipindi chote alichoitumikia tangu alipoajiunga nayo Januari mwaka jana akitokea Forest Rangers ya Zambia.

Huyo ni nyota wa pili kuachwa na Matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam msimu huu baada ya hapo awali kuachana na kiungo wake Frank Domayo ‘Chumvi’.

KISA MVUA TU…FAINALI ZA AFCON ZASOGEZWA MBELE…SASA KUPIGWA MWAKA 2024 BADALA YA 2023 KAIZER CHIEFS YAWAACHIA SIMBA KIUNGO MKENYA…KISA KOMBE LA FA…GSM AWAMIMIIA MASTAA YANGA MAMILIONI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply