Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA ISHU YA MANARA …JEMEDARI SAIDI AMVAA INJINI HERSI…AMPONDA...

BAADA YA KUMALIZANA NA ISHU YA MANARA …JEMEDARI SAIDI AMVAA INJINI HERSI…AMPONDA KWA KUOMBA KURA NA KOMBE…


Mchambuzi wa Soka la Bongo kupitia Kituo cha Radio EFM Jemedari Said Kazumari, amepinga utaratribu uliochukuliwa na Mgombea pekee wa nafasi wa Urais wa Klabu ya Young Africans Hersi Said, ya kwenda Studio za Wasafi FM akiwa na Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22.

Mapema leo Jumatano (Julai 06), Hersi Said alihojiwa kwenye kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM, kwa lengo la kunadi sera zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Young Africans utakaofanyika Jumamosi (Julai 09) jijini Dar es salaam.

Katika mahojiano hayo, Hersi alionekana akiwa na Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22, kitendo ambacho kimepigwa na Jemedari Said kufuatia andiko lake alilolichapisha kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii.

Jemedari ameandika: Tukisema tunaonekana wabaya au tuna chuki, mgombea ameenda kuomba kura akiwa na kombe la ubingwa.

Kwahiyo Klabu imetoa authorization kwamba huyu ndiyo Rais na sio mgombea.

Kama hivyo ndivyo manake wale alowataja akiwaombea kura  jana ama kuongozana nae nao wamebarikiwa na klabu?

Huu uchaguzi una ukiukwaji mkubwa sana ila kwakuwa tu watu wengi ni waoga wanaishia kusemea pembeni.

Kombe ni mali ya klabu haipaswi kutumika na mtu (mgombea) mmoja katika kutafuta namna ya kuingia madarakani, hatakama uko peke yako, inawezekana bado wapiga kura wangeweza kupiga kura za hapana. Unaenda na kombe ili kuonyesha nini?

Jana nilimsikia Afisa mhamasishaji kwamba hajaenda kwenye kampeni za marafiki zake kwakuwa yeye kama sehemu ya sekretarieti hawapaswi kuwa na upande.

Busara hiyo hiyo ya sekretaieti ingetumika kumnyima kombe mgombea. Ila kwakuwa tunaishi kwenye nchi ambayo UCHAWA ndiyo kilakitu tunaona kawaida tu.

NB: Huwezi kuelewa hii kama akili yako inatosha kuingia chooni ukatoka hujajichafua.

SOMA NA HII  YANGA SC YASHEREKEA UBINGWA..."SIMBA WATAKIMBIA UWANJANI...WALITUFUNGA MIDOMO