Habari za michezo

ACHANA NA KYOMBO ALIYETAMBULISHWA LEO…VIFAA VINGINE VIPYA KWA SIMBA HIVI HAPA…WEKA BANDO LA KUTOSHA…

admin July 9, 2022 12:21 pm


HATIMAYE, Simba imepata saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Habib Kyombo kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kutokea sintofahamu hapo awali.

Awali nyota huyo alidaiwa kusaini timu mbili tofauti akianza na wageni wa Ligi Kuu Bara Singida Big Stars kisha kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kukubali dili jipya la kujiunga na Simba.

Wakati akiitumikia Mbeya Kwanza katika msimu ulioisha Juni 29, mwaka huu staa huyo alifunga mabao sita ya Ligi Kuu Bara katika mechi 15 alizocheza na kikosi hicho ambacho  kimeshuka daraja baada ya matokeo mabovu.

Huu ni usajili wa kwanza Simba kwa wachezaji wazawa msimu huu baada ya ule wa Moses Phiri raia wa Zambia aliyejiunga na miamba hiyo Juni 15 akitokea klabu ya Zanaco ya huko nchini kwao Zambia.

Mbali na Usajili huo ila  nyota wengine ambao wamejiunga na miamba hiyo ni Victor Akpan kutoka Coastal Union, Cesar Manzoki (Vipers FC), Nelson Okwa (Rivers United) na Augustine Okrah aliyetokea Asante Kotoko.

KICHUYA AFUNGUKA A-Z KUHUSU DILI LAKE NA SIMBA KWA MSIMU UJAO…”WANANIAMBIA KARIBU NYUMBANI”…. FAMILIA WAANIKA KILICHOMUUA BI HINDU….ALIKUWA AKIPUMULIA MASHINE NYUMBANI…”ALIKUWA NA WATU WENGI”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply