Habari za michezo

MIDO WA NEWCASTLE YA UINGEREZA ATAMBULISHWA YANGA… UKUMBI WALIPUKA KWA SHANGWE…

admin July 9, 2022 3:54 pm


RAIS mteule wa klabu ya Yanga, Hersi Said amemtambulisha rasmi kiungo aliyewahi kucheza Newcastle United ya Uingereza, Gael Bigirimana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere unapofanyika uchaguzi wa timu hiyo.

Akizungumza mbele ya wajumbe, Hersi amesema mchezaji huyo ana sifa kubwa kwani amecheza katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Hersi amesema wao wanasajili wachezaji wazuri na ndio maana wamemchukua mchezaji  wa zamani wa klabu ya Newcastle iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu nchini Uingereza.

“Sisi tunasajili na tumeahidi kabisa kushusha vifaa, huyu hajacheza timu ndogo bali amecheza timu kubwa na kwenye Ligi Kubwa,” amesema Hersi na kuongeza;

“Wanasema eti Mayele ataenda Kaizer Chiefs, sisi wenyewe tunachukua wachezaji kwao huko.”

Hersi amesema wamefanya usajili wa wachezaji watano wa nguvu na watendelea kuwatambulisha mpaka wanamaliza.

“Kuna mchezaji tutamtambulisha leo usiku saa tisa, mwingine ataingia Jumatatu, huyu wa Jumatatu amecheza Ligi ya Spain,” amesema Hersi.

Yanga mpaka sasa imewatambulisha rasmi, Lazarous Kambole, Benard Morrison na Gael Bigirimana.

UCHAGUZI MKUU YANGA : MANARA AMPA INJINIA HERSI MIAKA MITATU ….SENZO ABARIKI JAMBO LIENDELEE… CHUMA HIKI HAPA…KIUNGO WA NEWCASTLE ATAMBULISHWA YANGA..MWINGINE WA LA LIGA KUTUA…HERSI AANZA NA MAMBO 6…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply