Simba SC. imesaini mkataba wa udhamini wa miaka mitano na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET ambayo sasa ni Mdhamini Mkuu wa Club hiyo kuanzia July 1 2022.
Taarifa ya Simba SC. imesema taarifa kamili juu ya udhamini huu zitatolewa na pande zote mbili siku ya Jumatatu August 1 2022.
Kabla ya M-BET Timu ya Simba ilikuwa na mkataba wa udhamini na Kampuni ya kubashiri ya Sport Pesa.
Tarifa za ndani zinasema kuwa kwenye mkataba huo , M-BET watailipa Simba Bilioni tatu kwa mwaka , sawa na bilioni kumi na tano kwa miaka mitano.
Hata hivyo inafahamika vyema kuwa M-BET wamezishinda kampuni za Sport Pesa na Kampuni ya mtandao wa kijamii wa Tik-Tok ambapo waraka wa siri kutoka ndani ya klabu hiyo unadai kuwa SportPesa ambao wataongeza mkataba na Yanga hivi karibuni wao waliweka mezani Bilioni Mbili. huku Tik-Tok wakiiweka mezani ofa ya bilioni mbili na nusu kwa mwaka.
Kwa mkataba huo simba kwa mwaka inauhakika wa kukusanya zaidi ya Bilioni nne kutoka kwa wadhamini wake, huku Vunja bei wakitoa Bilioni moja na sasa M-Bet nao wakitoa bilioni tatu, hapo ukicha mikataba mingine kama Air Tanzania, Emirates na Metl ambapo ukikusanya unakuta Simba wakipata zaidi ya Bilioni nne mpaka tano kwa mwaka.