Habari za michezo

ZORAN : TIMU YENYE MALENGO MAKUBWA HUWAPA MAKOCHA MKATABA MREFU…SIMBA WAMENIPA MWAKA MMOJA TU…

admin July 14, 2022 10:15 am


KOCHA mpya wa Simba, Zoran Manojlovic amesema mkataba wa mwaka mmoja aliopewa na uongozi wa timu hiyo sio kitu kibaya kwake kwani sehemu zingine wanatoa mkataba wa miezi sita.

Zoran amesema hayo wakati akitambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa babari, Zoran amesema kwa uzoefu wake wa kuishi Ulaya, timu yenye malengo makubwa inawapa makocha wake mikataba ya miaka angalau minne jambo ambalo ni tofauti na Afrika.

“Nina uzoefu wa soka la Afrika huwa wanatoa mkataba wa miezi sita, huu wa mwaka mmoja ni mzuri japokuwa itanichukua hata miezi sita kwanza kujua namna ambavyo soka la hapa linavyokwenda,” amesema Zoran.

Zoran amesema anaifahamu Simba baada ya kuiona kwenye Mashindano ya CAF na hata aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Didier Gomes alikuwa anamfatilia vizuri.

“Naijua Simba kwa sababu nimeona mechi zao za CAF, Yanga naijua kidogo sana maana sijawahi kuona mechi zao,” amesema Zoran na kuongeza;

“Kocha wa zamani Simba, Didier (Gomes) nilikuwa nae Ligi ya Sudan na nilimfungua ila ni kocha mzuri sana,” amesema Zoran.

Zoran amepita katika timu mbalimbali Afrika kama Wydad Ac (Morocco), Al Hilal (Sudan), na CR Belouizdad 

M-BET WADHAMINI WAPYA SIMBA….WAZISHINDA TIK-TOK NA SportsPesa…MKATABA WAO NI ZAIDI YA KUFRU AISEE… NDEMLA AZIDI KUJICHIMBIA MIKOANI….SINGIDA BIG STARS WAMCHOTA JUU KWA JUU KWA DAU NONO…ASALIMU AMRI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply