Habari za michezo

NDEMLA AZIDI KUJICHIMBIA MIKOANI….SINGIDA BIG STARS WAMCHOTA JUU KWA JUU KWA DAU NONO…ASALIMU AMRI…

admin July 14, 2022 10:24 am


Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Simba SC, Said Ndemla ambaye alimalizia msimu akiitumikia klabu ya Mtibwa Sugar kwa mkopo tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya Singida Big Stars ambayo imepanda ligi kuu msimu ujao.

Timu hiyo ambayo zamani ilijulikana kama Dtb imemsainisha kiungo huyo wa ushambuliaji mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru akiwa amemaliza mkataba wake wa miaka miwili katika klabu ya Simba sc ambayo ilimtoa kwa mkopo kwenda Mtibwa sugar kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Azam Fc inatajwa nayo ilikuwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo lakini kwa taarifa hizi inaonekana Azam Fc imezidiwa kete na Singida Big Stars katika kumsainisha mkataba staa huyo ambaye amekulia Simba SC akianza kuichezea tangu katika kikosi cha vijana kilichotikisa miaka hiyo kikiwa na vijana kama Jonas Mkude,Ramadhani Singano na wengineo.

ZORAN : TIMU YENYE MALENGO MAKUBWA HUWAPA MAKOCHA MKATABA MREFU…SIMBA WAMENIPA MWAKA MMOJA TU… AMKENI AMKENI…WAMEMRUDISHA TENA TSHISIMBI LIGI KUU…KAPEWA MIAKA MIWILI YA NGUVU KUKIPIGA MSIMU UJAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply