Habari za michezo

AMKENI AMKENI…WAMEMRUDISHA TENA TSHISIMBI LIGI KUU…KAPEWA MIAKA MIWILI YA NGUVU KUKIPIGA MSIMU UJAO…

admin July 14, 2022 10:42 am


Timu ya Ihefu FC imekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa zamani wa Yanga, Papy Tshisimbi kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kitayosce huku akichimba mkwara kwamba ametua kwa kazi moja tu.

Tshishimbi pamoja na kutua timu ambayo imetoka daraja la chini na kupanda Ligi Kuu, amekiri kujivunia kuzoea soka la Tanzania huku akiahidi mambo makubwa zaidi.

Akizungumza Tshishimbi alisema malengo yake ya kurudi ligi kuu yametimia kwani alikuwa ameikumbuka mikikimikiki ya timu kubwa kama Simba na Yanga baada ya kushuka hadi Ligi ya Championship akiitumikia Kitayosce.

“Nawashukuru viongozi kwa kuonyesha nia ya kuwa na mimi kwenye kikosi chao msimu ujao, haikuwa rahisi ila ninachoweza kuwaahidi ni kuwapa furaha iliyowafanya kunileta hapa, nina uzoefu na ligi kuu hilo nililidhihilisha nikiwa Yanga,” alisema Tshishimbi na kuongeza;

“Nawaheshimu wachezaji niliowakuta kwenye timu hiyo sio wageni kwangu tumekutana kwenye michezo ya Championship natarajia ushirikiano mzuri ili kufikia malengo tukiwa pamoja.”

Tshishimbi ambaye kwenye ligi hiyo amefunga mabao mawili, aliongeza kuwa kutua kwake Ihefu ni mwanzo wa kurudisha imani yake kwa wadau wa soka ambao wanaamini kuwa ameshuka kiwango baada ya kuibukia Kitayosce ambayo imekosa nafasi ya kupanda msimu huu.

NDEMLA AZIDI KUJICHIMBIA MIKOANI….SINGIDA BIG STARS WAMCHOTA JUU KWA JUU KWA DAU NONO…ASALIMU AMRI… KISA SIMBA…OKRAH AFUNGUKA ALIVYOZOZANA NA MABOSI ZAKE GHANA…ADAI WALITAKA KUMBANIA ASIJE TZ…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply