Habari za michezo

KISA SIMBA…OKRAH AFUNGUKA ALIVYOZOZANA NA MABOSI ZAKE GHANA…ADAI WALITAKA KUMBANIA ASIJE TZ…

admin July 14, 2022 10:43 am


Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba SC, Augustine Okrah amefanya mahojiano ya kwanza na Msemaji wa Klabu hiyo Ahmed Ally mara baada ya kutua jijini Dar ambapo ameeleza jinsi ilivyokuwa ngumu kuamua kuichezea Simba.

Amesema, alipoletewa ofa na Simba, alivutana na uongozi wake wakaanza kuvutana lakini mwisho wa siku walikubaliana na uamuzi wake wa kuwachagua Wekundu hao wa Msimbazi.

“Haikuwa rahisi, tulivutana sana na uongozi wangu lakini baadaye walikubaliana na chaguo langu la kuja Simba,” alisema Okrah.

Nyota huyo ametua Msimbazi na kupewa mkataba wa miaka miwili ambapo leo Julai 14, 2022 anatarajia kukwea pipa na wachezaji wenzake kuelekea nchini Misri kwa ajili kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

AMKENI AMKENI…WAMEMRUDISHA TENA TSHISIMBI LIGI KUU…KAPEWA MIAKA MIWILI YA NGUVU KUKIPIGA MSIMU UJAO… MSUVA AFUNGUKA MAZITO ALIYOFANYIWA NA WAARABU….ADAI ANAPACHUKIA SANA MOROCCO….”WALINIFUNGIA….”

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply