Habari za michezo

MSUVA AFUNGUKA MAZITO ALIYOFANYIWA NA WAARABU….ADAI ANAPACHUKIA SANA MOROCCO….”WALINIFUNGIA….”

admin July 14, 2022 4:35 pm

Aliyekuwa mchezaji wa Wydad Casablanca ya Morocco, Simon Happygod Msuva amesema kwa sasa hataki tena kurudi kucheza soka nchini humo huku akiongeza kuwa hataki kabisa kusikia habari za Wydad.

kauli hiyo ya Msuva inakuja baada ya kuwashtaki Wydad kwa kukiuka masharti ya mkataba wake huku akishinda kesi hiyo FIFA na Wydad kuamriwa wamlipe pesa anazowadai kiasi cha Tsh bilioni 1.6.

“Morocco sitaki hata kupasikia. Kiukweli siwezi na sitaki kurudi tena Morocco. Ni mtu mmoja tu amesababisha mimi nipachukie Morocco ambaye ni Rais wa Wydad Casablanca (Said Naciri). Ilifika steji wakafunga akaunti zangu za benki,” amesema Msuva.

Sasa Msuva yuko huru kujiunga na timu yoyote huku Yanga ikitajwa kumnyemelea staa wao aliyemaliza msimu wake wa mwisho Jangwani akiwa mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 14.

KISA SIMBA…OKRAH AFUNGUKA ALIVYOZOZANA NA MABOSI ZAKE GHANA…ADAI WALITAKA KUMBANIA ASIJE TZ… GEITA GOLD WASALIMU AMRI KWA NDAYIRAGIJE…WATII AGIZO LA FIFA BILA MAKEKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply